آنگاه آدم از پروردگارش کلماتی فراگرفت [و درخواستِ بخشایش نمود] و الله توبۀ او را پذیرفت؛ زیرا الله، توبهپذیرِ مهربان است.
تفاسیر
لایهها
درس ها
بازتاب ها
پاسخها
قیراط
حدیث
Ādam alipokea matamko ya kuomba ili akubaliwe, aliyoletewa na Mwenyezi Mungu, kwa njia ya ilham (ilham), yaliyokusanya toba na kutaka msamaha, nayo ni neno Lake Aliyetukuka, “Ewe Mola wetu! Tumejidhulumu nafsi zetu. Na Usipotusamehe na Kuturehemu, hakika tutakuwa ni miongoni mwa waliyopata hasara.” (23). Mwenyezi Mungu Alikubali toba yake na Akamsamehe. Kwani Yeye, Aliyetukuka, ni Mwingi wa kukubali toba ya Mwenye kutubia miongoni mwa waja Wake na ni Mwenye Kuwarehemu.