[الله] فرمود: «ای موسی، [بدان که] من تو را به پیامها و کلام [بیواسطۀ] خویش، بر مردمان برگزیدم. آنچه به تو میبخشم بگیر و سپاسگزار باش».
تفاسیر
لایهها
درس ها
بازتاب ها
پاسخها
قیراط
حدیث
Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Mūsā, Mimi nimekuchagua kati ya watu kwa ujumbe wangu kwa viumbe wangu niliokutuma kwao na kwa kusema kwangu na wewe pasi na mtu wa kati. Basi chukua niliyokupa kati ya maamrisho yangu na makatazo yangu, ushikamane nayo na uyatumie na uwe ni miongoni mwa wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa utume aliokupa na Akakuhusu kwa maneno Yake.