Et entre les deux, il y aura un mur, et, sur Al-A'râf seront des gens qui reconnaîtront tout le monde par leurs traits caractéristiques . Et ils crieront aux gens du Paradis : "Paix sur vous !" Ils n’y sont pas entrés bien qu’ils le souhaitent. 1
Tafsirs
Niveaux
Leçons
Réflexions
Réponses
Qiraat
Hadith
Na baina ya watu wa Peponi na watu Motoni patakuwa na kizuizi kikubwa kinaitwa Al-A’rāf. Na juu ya kizuizi hiki kutakuwa na wanaume wanaowajuwa watu wa Peponi na watu wa Motoni kwa alama zao kama weupe wa nyuso za watu wa Peponi na weusi wa nyuso za watu wa Motoni. Wanaume hawa ni watu ambao vitendo vyao vizuri na viovu viko sawasawa, na wao wana matumaini ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Wanaume hao wa hapo Al-A’rāf watawaita watu wa Peponi kwa maamkuzi wakiwaambia, «Salamun 'alaykum»(Amani iwe juu yenu.) Watu hawa wa Al-A’rāf bado hawajaingia Peponi, na wao wana matumaini ya kuingia.