Maka Kami kirimkan kepada mereka topan, belalang, kutu, katak dan darah (air minum berubah menjadi darah) sebagai bukti-bukti yang jelas, tetapi mereka tetap menyombongkan diri dan mereka adalah kaum yang berdosa.
Tafsir
Lapisan
Pelajaran
Refleksi
Jawaban
Qiraat
Hadits
Tukawapelekea wao mafuriko yenye kumaliza yaliyozamisha makulima na matunda; tukapeleka nzige wakazila nafaka zao, matunda yao, milango yao, sakafu zao na nguo zao; na tukapeleka chawa wanaoharibu matunda na kumaliza wanyama na mimea; tukapeleka vyura wakajaa kwenye vyombo vyao na vyakula vyao na malazi yao; na pia tukapeleka damu, ikawa mito yao na visima vyao vimegeuka damu, wasipate maji safi ya kunywa. Hii ni miujiza kati ya miujiza ya Mwenyezi Mungu, hakuna aiwezae isipokuwa Yeye, baadhi yake imetengwa na mingine. Pamoja na haya yote, watu wa Fir'awn walijiona watukufu, wakafanya kiburi kwa kukataa kumuamini Mwenyezi Mungu, wakawa ni watu wanatenda mambo Anayoyakataza Mwenyezi Mungu ya maasia na uhalifu kwa, ujeuri na uasi.