Sesungguhnya orang-orang yang bertaqwa, apabila mereka disentuh oleh sesuatu imbasan hasutan dari Syaitan, mereka ingat (kepada ajaran Allah) maka dengan itu mereka nampak (jalan yang benar).
Tafsir
Lapisan
Pelajaran
Renungan
Jawapan
Qiraat
Hadis
Hakika wale wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe wake, kwa kuogopa mateso Yake kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kuyaepuka makatazo Yake, likiwapata tukio lolote la wasiwasi wa Shetani, wanayakumbuka yale Aliyowalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao ya kumtii na kutubia Kwake, na punde si punde wanakomeka na kumuasi Mwenyezi Mungu wakiwa kwenye hoja ya wazi, wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na wenye kumuasi Shetani.