Dan berapa banyak negeri yang Kami binasakan, iaitu datang azab seksa Kami menimpa penduduknya pada malam hari, atau ketika mereka berehat pada tengah hari.
Tafsir
Lapisan
Pelajaran
Renungan
Jawapan
Qiraat
Hadis
Na miji mingi tuliwaangamiza watu wake kwa sababu ya kwenda kinyume kwao na Mitume wetu na kuwakanusha. Hilo likawaletea utwevu wa duniani uliounganishwa na unyonge wa Akhera. Basi adhabu yetu iliwajia, wakati mwingine wakiwa wamelala usiku, na wakati mwingine wakiwa wamelala mchana. Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuwa ni nyakati za utulivu na mapumziko. Hivyo basi, kuja kwa adhabu kwenye nyakati mbili hizi kunababaisha zaidi na adhabu yenyewe huwa ni kali zaidi.