De eerste van hen zal tegen de laatste van hen zeggen: “Jullie waren niet beter dan ons, proef dus de bestraffing die jullie verdienen.”
Tafseers
Lagen
Lessen
Reflecties
Antwoorden
Qiraat
Hadith
Hapo watasema wale waliofuatwa miongoni mwa viongozi na wengineo kuwaambia wafuasi wao, «Sisi na nyinyi tuko sawa katika uharibifu na upotevu na katika kufanya vitendo ambavyo ndio sababu ya kupata adhabu, kwa hivyo, nyinyi hamuna ubora juu yetu.» Mwenyezi Mungu Atawaambia wao wote, «Basi ionjeni adhabu,» yaani adhabu ya Jahanamu «kwa makosa mliyoyatenda.»