Ó fiéis, quando fordes convocados, para a Oração da Sexta-feira, recorrei à recordação de Deus e abandonai os vossosnegócios; isso será preferível, se quereis saber.
Tafsirs
Camadas
Lições
Reflexões
Respostas
Qiraat
Hadith
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, endeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha nyinyi na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu nyinyi kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Basi iwapo nyinyi mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo. Kwenye aya hii kuna dalili kwamba kwenda kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima.