Não reparam no reino dos céus e da terra e em tudo quando Deus criou e em que, quiçá, seu fim se aproxima? E quemensagem, depois desta (Alcorão), crerão?
Tafsirs
Camadas
Lições
Reflexões
Respostas
Qiraat
Hadith
Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Mwenyezi Mungu, kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu, zimetukuka sifa Zake, kwenye vitu viwili hivyo, wakalitia akilini hilo na wakalizingatia kwa akili zao na wakaangalia muda wa kikomo cha maisha yao ambao huenda ukawa umesongea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi?