E se não lhes apresentas um sinal, dizem-te: Porque não o inventas? Dize: Eu não faço mais do que seguir o que merevela o meu Senhor. Este (Alcorão) encerra discernimentos do vosso Senhor e é, por isso, orientação e misericórdia paraos que crêem.
Tafsirs
Camadas
Lições
Reflexões
Respostas
Qiraat
Hadith
Na usipowajia, ewe Mtume, washirikina hawa na aya wanasema, «Si uitunge na uizue wewe mwenyewe.» Waambie, ewe Mtume, «Hili si langu, na haifai kwangu mimi nilifanye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameniamuru kufuata wahyi nilioletewa kutoka Kwake. Nao ni hii Qur’ani ninayowasomea, inayokusanya hoja na dalili zinazotoka kwa Mola wenu na yenye ufafanuzi, inayoongoza Waumini kwenye njia iliyolingana sawa, na ni rehema ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawarehemu waja Wake Waumini.