Da terra fértil brota a vegetação, com o beneplácito do seu Senhor; da estéril, porém, nada brota, senão escassamente. Assim elucidamos os versículos para os agradecidos.
Tafsirs
Camadas
Lições
Reflexões
Respostas
Qiraat
Hadith
Na ardhi nzuri, ikiteremkiwa na mvua, inatoa mimea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake, ikiwa mizuri na kwa njia ya wepesi. Hivyo ndivyo alivyo Muumini, zikiteremka aya za Mwenyezi Mungu kwake, hunufaika nazo na huzalisha kwake maisha mema. Ama ardhi ya chumvi iliyo mbovu; hiyo haitoi mimea isipokuwa mibovu isiyokuwa na faida, tena kwa shida, na haitoi mimea mizuri. Hivyo ndivyo alivyo kafiri, hanufaiki kwa aya za Mwenyezi Mungu. Mfano wa sampuli hiyo nzuri katika kueleza, ndiyo namna tunavyoleta hoja na dalili mbalimbali kuthibitisha haki kwa watu wanaozishukuru neema za Mwenyezi Mungu na wanaomtii.