Jamais enviamos um profeta a cidade alguma, sem antes afligirmos os seus habitantes com a miséria e adversidade, a fimde que se humilhem.
Tafsirs
Camadas
Lições
Reflexões
Respostas
Qiraat
Hadith
Na hatukumtuma Nabii kwenye kijiji chochote kuwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuwakataza ushirikina ambao wanao, kisha wakamkanusha, isipokuwa tuliwapa mtihani wa shida na mikasa, tukawatia kwenye miili yao magonjwa na ndwele, na katika mali yao ufukara na uhitaji, kwa matumaini kwamba wanyenyekee, waelekee kwa Mwenyezi mungu na warudi kwenye haki.