Мы спасли его и тех, кто был с ним, по Своей милости и искоренили тех, которые сочли ложью Наши знамения и не стали верующими.
Тафсиры
Слои
Уроки
Размышления
Ответы
Кираат
Хадис
Basi adhabu ya Mwenyezi Mungu ikatukia kwa kutumwa upepo mkali juu yao. Mwenyezi Mungu akamuokoa Hūd na walioamini pamoja na yeye kwa rehema kubwa kutoka kwake, Aliyetukuka. Na Akawaangamiza makafiri wote miongoni mwa watu wake, Akawavunjavunja mpaka wa mwisho wao. Na wao hawakuwa ni Waumini kwa kuwa walikusanya baina ya kukanusha aya za Mwenyezi Mungu na kuacha kufanya vitendo vyema.