Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:26

10:26
۞ للذين احسنوا الحسنى وزيادة ولا يرهق وجوههم قتر ولا ذلة اولايك اصحاب الجنة هم فيها خالدون ٢٦
۞ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ ٱلْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌۭ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌۭ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٢٦
۞ لِّلَّذِينَ
أَحۡسَنُواْ
ٱلۡحُسۡنَىٰ
وَزِيَادَةٞۖ
وَلَا
يَرۡهَقُ
وُجُوهَهُمۡ
قَتَرٞ
وَلَا
ذِلَّةٌۚ
أُوْلَٰٓئِكَ
أَصۡحَٰبُ
ٱلۡجَنَّةِۖ
هُمۡ
فِيهَا
خَٰلِدُونَ
٢٦
Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ni ya Waumini, waliofanya vizuri kumuabudu Mwenyezi Mungu,wakamtii katika yale Aliyowaamrisha na Akayakataza, Pepo na zaidi yake ambayo ni kuutazama Uso wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, huko Peponi, na kupata msamaha na radhi. Na wala nyuso zao hazitafinikwa na vumbi wala unyonge kama itakavyo kuwapata watu wa Moto. Hawa wanaosifika na sifa hizi ndio watu wa Peponi, ni wenye kukaa milele kabisa humo.