Hao ndio Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao ndio walio ghafilika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapiga muhuri nyoyo zao kwa ukafiri na ufadhilishaji dunia juu ya Akhera, hazitafikiwa na nuru ya uongofu, na Amewafanya viziwi masikio yao kutozisikia aya za Mwenyezi Mungu , kusikia kwa kuzingatia, na Amewafanya vipofu macho yao wasizione hoja zinazojulisha uungu wa Mwenyezi Mungu , na hao ndio wenye kughafilika na ile adhabu Aliyowaandalia Mwenyezi Mungu.