Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:43

16:43
وما ارسلنا من قبلك الا رجالا نوحي اليهم فاسالوا اهل الذكر ان كنتم لا تعلمون ٤٣
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًۭا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۚ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ٤٣
وَمَآ
أَرۡسَلۡنَا
مِن
قَبۡلِكَ
إِلَّا
رِجَالٗا
نُّوحِيٓ
إِلَيۡهِمۡۖ
فَسۡـَٔلُوٓاْ
أَهۡلَ
ٱلذِّكۡرِ
إِن
كُنتُمۡ
لَا
تَعۡلَمُونَ
٤٣
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hatukuwatuma kwa waliotangulia kabla yako, ewe Mtume, isipokuwa Mitume miongoni mwa wanaume, sio Malaika, tunaowaletea wahyi. Na iwapo nyinyi, enyi washirikina wa Kikureshi, hamliamini hilo, basi waulizeni waliopewa vitabu vilivyopita, watawapa habari kwamba Manabii walikuwa ni binadamu, mkiwa hamjui kwamba wao ni binadamu. Aya hii inakusanya kila suala kati ya masuala ya Dini, iwapo mtu hana ujuzi nalo amuulize anayelijua miongoni mwa wanavyuoni waliovama katika elimu.