Na ni vyake Yeye viliomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je! Mtamcha mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na ni vya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuviendesha. Na ibada inaelekezwa Kwake PekeYake, na pia kutiiwa na kutakaswa daima. Basi je, inafaa kwenu nyinyi mumuogope asiyekuwa Yeye na mumuabudu?