Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:56

16:56
ويجعلون لما لا يعلمون نصيبا مما رزقناهم تالله لتسالن عما كنتم تفترون ٥٦
وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًۭا مِّمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ ۗ تَٱللَّهِ لَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ ٥٦
وَيَجۡعَلُونَ
لِمَا
لَا
يَعۡلَمُونَ
نَصِيبٗا
مِّمَّا
رَزَقۡنَٰهُمۡۗ
تَٱللَّهِ
لَتُسۡـَٔلُنَّ
عَمَّا
كُنتُمۡ
تَفۡتَرُونَ
٥٦
Na hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu ya tunavyo waruzuku.Wallahi! Bila ya shaka mtasailiwa kwa hayo mliyo kuwa mnayazua! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na miongoni mwa uovu wa matendo yao ni kwamba wao wanawatengea masanamu waliowafanya ni waungu, wasiojua chochote na wasionufaisha wala kudhuru, sehemu ya mali zao walizoruzukiwa na Mwenyezi Mungu ili kujisongeza kwao. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Mtaulizwa tena mtaulizwa Siku ya Kiyama kuhusu yale ya urongo ambayo mlikuwa mkimzulia Mwenyezi mungu.