Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliyetakasika! Na wao wenyewe, ati ndio wawe na hayo wanayo yatamani! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na makafiri wanamsingizia Mwenyezi Mungu kuwa ana watoto wa kike na huwa wakisema, «Malaika ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu». Ameepukana Mwenyezi Mungu na neno lao. Na wanajichukulia wao wenyewe watoto wa kiume wanaowapenda.