Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mūsā akamjibu, «Umeshajua kwa yakini, ewe Fir'awn, kwamba hakuiteremsha miujiza hiyo tisa yenye kuutolea ishahidi unabii wangu isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi, ipate kuwa ni dalili ambazo wenye busara watazitumia kuonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika uola Wake na uungu Wake, na mimi nina yakini kwamaba wewe, ewe Fir'awn, ni mwenye kuangamia, kulaaniwa na kushindwa.»