Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Bani Israil 17:51

17:51
او خلقا مما يكبر في صدوركم فسيقولون من يعيدنا قل الذي فطركم اول مرة فسينغضون اليك رءوسهم ويقولون متى هو قل عسى ان يكون قريبا ٥١
أَوْ خَلْقًۭا مِّمَّا يَكْبُرُ فِى صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ قُلِ ٱلَّذِى فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍۢ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبًۭا ٥١
أَوۡ
خَلۡقٗا
مِّمَّا
يَكۡبُرُ
فِي
صُدُورِكُمۡۚ
فَسَيَقُولُونَ
مَن
يُعِيدُنَاۖ
قُلِ
ٱلَّذِي
فَطَرَكُمۡ
أَوَّلَ
مَرَّةٖۚ
فَسَيُنۡغِضُونَ
إِلَيۡكَ
رُءُوسَهُمۡ
وَيَقُولُونَ
مَتَىٰ
هُوَۖ
قُلۡ
عَسَىٰٓ
أَن
يَكُونَ
قَرِيبٗا
٥١
Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Au kuweni umbo lolote kubwa ambalo akili zenu zaliona kuwa liko mbali na uhakika.» Na watasema kwa kukanusha, «Ni nani atakayeturudisha kwenye uhai baada ya kufa?» Waambie, «Atakayewarudisha na kuwarejesha ni Mwenyezi Mungu Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako mara ya kwanza.» Na wasikiapo majibu haya watatikisa vichwa vyao kwa njia ya shere, huku wakiona ajabu na watasema, wakiliona jambo hilo kuwa ni mbali kukubalika, «Ufufuzi huu utatukia lini?» Sema, «Ni lipi linalowajulisha kwamba Ufufuzi huu, mnaoukanusha na mnaouona kuwa uko mbali, huenda ukawa ni wenye kutukia kipindi cha karibu?»