Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Miongoni mwa sifa za hawa wenye kusubiri ni kwamba wao wanapofikwa na kitu wanachokichukia husema, «Sisi ni waja waliomilikiwa na Mwenyezi Mungu, tunaoendeshwa kwa amri Yake na mapitisho Yake. Anafanya kwetu Alitakalo. Na sisi Kwake, Peke Yake, ni wenye kurudi kwa kufa, kisha kwa kufufuliwa ili kuhesabiwa na kulipwa.