Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi ambao mumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mukaifuata Sheria Yake kivitendo, Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kufunga, kama Alivyowafaradhia uma waliokuweko kabla yenu, ili mupate kumcha Mola wenu na kuweka kinga kati yenu na maasia, kwa kumtii na kumuabudu Peke Yake.