Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:2

2:2
ذالك الكتاب لا ريب فيه هدى للمتقين ٢
ذَٰلِكَ ٱلْكِتَـٰبُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًۭى لِّلْمُتَّقِينَ ٢
ذَٰلِكَ
ٱلۡكِتَٰبُ
لَا
رَيۡبَۛ
فِيهِۛ
هُدٗى
لِّلۡمُتَّقِينَ
٢
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Qurani hii ni kitabu kisicho na shaka kuwa kinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Haifai kwa mtu yoyote kufanya shaka juu yake kwa uwazi wake. Wananufaika kwayo wenye uchajimungu (taqwā), wenye kujikinga kwa elimu yenye manufaa na amali njema, na wao ndio wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kufuata hukumu Zake.