Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na taja kwa watu, ewe Mtume, takrima ya Mwenyezi Mungu kwa Ādam Aliposema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kuwaambia Malaika, “Msujudieni Ādam kwa njia ya kumheshimu na kuonyesha fadhila zake.” Wote walitii amri, isipokuwa Iblisi alikataa kusujudu kwa sababu ya kiburi na uhasidi, akawa ni miongoni mwa wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, wenye kuasi amri Yake.