Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:41

2:41
وامنوا بما انزلت مصدقا لما معكم ولا تكونوا اول كافر به ولا تشتروا باياتي ثمنا قليلا واياي فاتقون ٤١
وَءَامِنُوا۟ بِمَآ أَنزَلْتُ مُصَدِّقًۭا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوٓا۟ أَوَّلَ كَافِرٍۭ بِهِۦ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِى ثَمَنًۭا قَلِيلًۭا وَإِيَّـٰىَ فَٱتَّقُونِ ٤١
وَءَامِنُواْ
بِمَآ
أَنزَلۡتُ
مُصَدِّقٗا
لِّمَا
مَعَكُمۡ
وَلَا
تَكُونُوٓاْ
أَوَّلَ
كَافِرِۭ
بِهِۦۖ
وَلَا
تَشۡتَرُواْ
بِـَٔايَٰتِي
ثَمَنٗا
قَلِيلٗا
وَإِيَّٰيَ
فَٱتَّقُونِ
٤١
Na aminini niliyo yateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo. Na niogopeni Mimi tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na iaminini Qur,ani, enyi wana wa Isrāīl, ambayo niliiteremsha kwa Muhammad, aliye Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, ambayo inalingana na yale mnayoyajua yaliyo sahihi katika Taurati. Na msiwe ni kundi la mwanzo la Watu wa Kitabu (ahl al-kitāb) kuikanusha. Na wala msizibadilishe aya zangu kwa thamani chache ya taka za dunia zenye kuondoka. Na Kwangu Mimi, Peke Yangu, fanyeni vitendo vya kunitii na acheni kuniasi.