Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:71

2:71
قال انه يقول انها بقرة لا ذلول تثير الارض ولا تسقي الحرث مسلمة لا شية فيها قالوا الان جيت بالحق فذبحوها وما كادوا يفعلون ٧١
قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌۭ لَّا ذَلُولٌۭ تُثِيرُ ٱلْأَرْضَ وَلَا تَسْقِى ٱلْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌۭ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا۟ ٱلْـَٔـٰنَ جِئْتَ بِٱلْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا۟ يَفْعَلُونَ ٧١
قَالَ
إِنَّهُۥ
يَقُولُ
إِنَّهَا
بَقَرَةٞ
لَّا
ذَلُولٞ
تُثِيرُ
ٱلۡأَرۡضَ
وَلَا
تَسۡقِي
ٱلۡحَرۡثَ
مُسَلَّمَةٞ
لَّا
شِيَةَ
فِيهَاۚ
قَالُواْ
ٱلۡـَٰٔنَ
جِئۡتَ
بِٱلۡحَقِّۚ
فَذَبَحُوهَا
وَمَا
كَادُواْ
يَفۡعَلُونَ
٧١
Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni Ng'ombe asiye tiwa kazini kulima Ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mūsā aliwaambia, “Mwenyezi Mungu Anasema kwamba huyo ni ng’ombe asiyetumiwa kwa kazi ya kulima ardhi ya kilimo, hakutayarishwa kutia maji, hana kasoro yoyote na hana alama yoyote ya rangi isiyokuwa rangi ya ngozi yake.” Wakasema, “Sasa umekuja na ukweli wa sifa ya ng’ombe.” Wakalazimika kumchinja baada ya muda mrefu wa mbinu za kuchelewesha. Na walikuwa karibu kutofanya hilo kwa ushindani wao. Hivi ndivyo walivyojitilia mkazo, ndipo Mwenyezi Mungu Akawafanyia mkazo.