Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: As-Sajdah 32:26

32:26
اولم يهد لهم كم اهلكنا من قبلهم من القرون يمشون في مساكنهم ان في ذالك لايات افلا يسمعون ٢٦
أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْقُرُونِ يَمْشُونَ فِى مَسَـٰكِنِهِمْ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ ۖ أَفَلَا يَسْمَعُونَ ٢٦
أَوَلَمۡ
يَهۡدِ
لَهُمۡ
كَمۡ
أَهۡلَكۡنَا
مِن
قَبۡلِهِم
مِّنَ
ٱلۡقُرُونِ
يَمۡشُونَ
فِي
مَسَٰكِنِهِمۡۚ
إِنَّ
فِي
ذَٰلِكَ
لَأٓيَٰتٍۚ
أَفَلَا
يَسۡمَعُونَ
٢٦
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwani haikuwabainikia hawa wenye kumkanusha Mtume ni mara ngapi tuliwaangamiza ummah waliotangulia kabla yao na huku wanatembea kwenye makazi yao, wakawa wanayaona waziwazi, kama vile watu wa Hūd, Ṣāliḥ na Lūṭ? Hakika katika hayo kuna alama na mawaidha ya kutolea ushahidi ukweli wa Mitume waliowajia na urongo wa ushirikina walionao. Basi kwani hawasikii, hawa wenye kuwakanusha Mitume, mawaidha ya Mwenyezi Mungu na dalili Zake wakapata kunufaika nayo?