Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mkidhihirisha chochote kwa ndimi zenu, enyi watu, kati ya vitu vinavyomkera Mtume katika vile alivyowakataza navyo au mkakificha ndani ya nafsi zenu, basi Mwenyezi Mungu, aliyetukuka anavijua vilivyomo ndani ya nyoyo zenu na vile mlivyovidhihirisha, na Atawalipa kwa hayo.