Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hii Qur’ani ni Teremsho linalotoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye kueneza rehema Zake kwa wema na waovu ulimwenguni, Mwenye kuhusisha rehema Zake kwa wema watupu kesho Akhera. Amemteremshia Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.