Huu ni uwongofu. Na wale wale walio zikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata adhabu inayo tokana na ghadhabu iliyo chungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwako, ewe Mtume, ni uongofu wenye kuondoa upotevu, ni dalili ya haki na inamuongoza kwenye njia iliyolingana sawa atakayeifuata na akaifanyia kazi. Na wale waliozikataa aya zilizomo ndani ya Qur’ani zenye kutolea dalili Ukweli na wasiziamini, watakuwa na adhabu miongoni mwa adhabu kali zaidi Siku ya Kiyama, yenye uchungu na kuumiza.