Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu anayaona myatendayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua yasioonekana ya mbinguni na ardhini, hakuna chochote kinachofichamana kwake katika hayo. Na Mwenyezi Mungu Anayaona matendo yenu na Atawalipa kwayo, yakiwa mema Atawalipa wema, na yakiwa maovu Atawalipa uovu.