Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anfal 8:28

8:28
واعلموا انما اموالكم واولادكم فتنة وان الله عنده اجر عظيم ٢٨
وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَآ أَمْوَٰلُكُمْ وَأَوْلَـٰدُكُمْ فِتْنَةٌۭ وَأَنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجْرٌ عَظِيمٌۭ ٢٨
وَٱعۡلَمُوٓاْ
أَنَّمَآ
أَمۡوَٰلُكُمۡ
وَأَوۡلَٰدُكُمۡ
فِتۡنَةٞ
وَأَنَّ
ٱللَّهَ
عِندَهُۥٓ
أَجۡرٌ
عَظِيمٞ
٢٨
Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mjue, enyi Waumini, kwamba mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu Amewapa jukumu la kuyasimamia, na watoto wenu ambao Mwenyezi Mungu Amewapa, ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni majaribio kwa waja Wake, ili Ajue: watamshukuru kwa neema hizo na kumtii au watashughulika nazo wamsahau Yeye? Na jueni kwamba mbele ya Mwenyezi Mungu kuna heri na thawabu kubwa kwa anayemcha na kumtii.