Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wakielekea kuacha vita na wakapendelea kuishi kwa amani na nyinyi, basi nawe elekea huko, ewe Nabii, na uyategemeze mambo yako kwa Mwenyezi Mungu na uwe na imani na Yeye. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kuyasikia maneno yao, Mwenye kuzijua nia zao.