Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:100

3:100
يا ايها الذين امنوا ان تطيعوا فريقا من الذين اوتوا الكتاب يردوكم بعد ايمانكم كافرين ١٠٠
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تُطِيعُوا۟ فَرِيقًۭا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَـٰنِكُمْ كَـٰفِرِينَ ١٠٠
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُوٓاْ
إِن
تُطِيعُواْ
فَرِيقٗا
مِّنَ
ٱلَّذِينَ
أُوتُواْ
ٱلۡكِتَٰبَ
يَرُدُّوكُم
بَعۡدَ
إِيمَٰنِكُمۡ
كَٰفِرِينَ
١٠٠
Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Imani yenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazitumia Sheria Zake kwa kuzifuata, iwapo mtalitii kundi la Mayahudi na Wanaswara, miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapa Taurati na Injili, watawapoteza na watawatia shaka katika dini yenu, ili mupate kurudi nyuma na kuikanusha haki baada ya kuwa mlikuwa waumini wa haki hiyo, basi msiwaamini juu ya dini yenu wala msiwakubalie rai yoyote au shauri.