Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kiweko miongoni mwenu, enyi Waumini, kikundi kitakacholingania katika kheri, kiamrishe mema, nayo ni yale yanayojulikana uzuri wake kisheria na kiakili, na kikataze maovu, nayo ni yale yanayojulikana uovu wake kisheria na kiakili. Na hao ndio watakaofaulu kupata Pepo zenye neema.