Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wala msiwe, enyi Waumini, kama waliopewa vitabu, ambao ulizuka uadui kati yao na kuchukiana, wakatengana makundi na vyama mbalimbali na wakatafautiana kwenye misingi ya dini yao baada ya haki kuwa wazi kwao. Na hao wanastahili adhabu kubwa iumizayo.