Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:106

3:106
يوم تبيض وجوه وتسود وجوه فاما الذين اسودت وجوههم اكفرتم بعد ايمانكم فذوقوا العذاب بما كنتم تكفرون ١٠٦
يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌۭ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌۭ ۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَـٰنِكُمْ فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ١٠٦
يَوۡمَ
تَبۡيَضُّ
وُجُوهٞ
وَتَسۡوَدُّ
وُجُوهٞۚ
فَأَمَّا
ٱلَّذِينَ
ٱسۡوَدَّتۡ
وُجُوهُهُمۡ
أَكَفَرۡتُم
بَعۡدَ
إِيمَٰنِكُمۡ
فَذُوقُواْ
ٱلۡعَذَابَ
بِمَا
كُنتُمۡ
تَكۡفُرُونَ
١٠٦
Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika (kuwa nyeusi). Ama hao ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Siku ya Kiyama zitakuwa nyeupe nyuso za watu wema ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata amri Yake; na zitakuwa nyeusi nyuso za watu waovu kati ya wale waliomkanusha Mtume Wake na wakaasi amri Yake. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi wataambiwa kwa kulaumiwa, «Je, mumekufuru baada ya kuamini kwenu, mkachagua ukafiri mkaacha Imani? Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri wenu.»