Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe kwa mn’garo wa neema na kwa yale mema ambayo walipewa bishara nayo, wao watakuwa katika Pepo ya Mwenyezi Mungu na starehe zake. Wao watasalia humo, hawatatoka humo milele.