Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hawatawadhuru nyinyi hawa watu waovu, miongoni mwa watu waliopewa Vitabu, isipokuwa kile kitakachoyaudhi masikizi yenu cha matamshi ya ushirikina na ukafiri na mengineyo. Na wakiwapiga vita, watashindwa na watakimbia hali ya kuwapa mgongo, kisha hawatapata ushindi juu yenu kwa hali yoyote.