Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:120

3:120
ان تمسسكم حسنة تسوهم وان تصبكم سيية يفرحوا بها وان تصبروا وتتقوا لا يضركم كيدهم شييا ان الله بما يعملون محيط ١٢٠
إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌۭ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌۭ يَفْرَحُوا۟ بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا ۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌۭ ١٢٠
إِن
تَمۡسَسۡكُمۡ
حَسَنَةٞ
تَسُؤۡهُمۡ
وَإِن
تُصِبۡكُمۡ
سَيِّئَةٞ
يَفۡرَحُواْ
بِهَاۖ
وَإِن
تَصۡبِرُواْ
وَتَتَّقُواْ
لَا
يَضُرُّكُمۡ
كَيۡدُهُمۡ
شَيۡـًٔاۗ
إِنَّ
ٱللَّهَ
بِمَا
يَعۡمَلُونَ
مُحِيطٞ
١٢٠
Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na miongoni mwa uadui wa watu hawa ni kwamba nyinyi, enyi Waumini, mpatwapo na jambo jema la ushindi au ngawira, wao hupatwa na butwaa na huzuni; iwapo mtapatwa na maudhi ya kushindwa au upungufu wa mali, watu na matunda, wao hulifurahia hilo. Na mkiwa na subira juu ya yaliyowafika na mkamuogopa Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha na Akawakataza nayo, hautawadhuru udhia wa vitimbi vyao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka yote wanayoyafanya hao makafiri ya uharibifu na Atawalipa kwayo.