Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:122

3:122
اذ همت طايفتان منكم ان تفشلا والله وليهما وعلى الله فليتوكل المومنون ١٢٢
إِذْ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ ١٢٢
إِذۡ
هَمَّت
طَّآئِفَتَانِ
مِنكُمۡ
أَن
تَفۡشَلَا
وَٱللَّهُ
وَلِيُّهُمَاۗ
وَعَلَى
ٱللَّهِ
فَلۡيَتَوَكَّلِ
ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
١٢٢
Makundi mawili miongoni mwenu yakaingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao; na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kumbuka, ewe Mtume, yale mambo yaliyowahusu kina Banū Salimah na Banū Ḥārithah wakati walipowaza kurudi nyuma, wao na kiongozi wao, mnafiki Abdullāh bin Ubayy bin Salūl, kwa kuogopa kukutana na adui. Lakini Mwenyezi Mungu Aliwalinda na Akawahifadhi wakaenda pamoja na wewe wakimtegemea Mwenyezi Mungu. Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na wajitegemeze Waumini.