Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Mwenyezi Mungu Aliwanusuru nyinyi, enyi Waumini, katika Badr juu ya maadui zenu washirikina pamoja na uchache wa idadi yenu na vifaa vyenu. Kwa hivyo, muogopeni Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, ili mpate kumshukuria neema Zake.