Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wanao shambulia kwa nguvu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ndio, unawatosha nyinyi msaada huu. Na kuna bishara nyingine kwenu, iwapo mtakuwa na subira ya kupambana na maadui zenu na mkamuogopa Mwenyezi Mungu kwa kuyatenda Aliyowamrisha na kuyaepuka Aliyowakataza. Na watakuja makafiri wa Maka kwa haraka kupigana na nyinyi, wakidhani kwamba wao watawamaliza. Mwenyezi Mungu Atawapa nyinyi msaada wa Malaika elfu tano wakiwa wamejitia alama zilizo wazi, wao na farasi wao.