Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua. Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Mwenyezi Mungu Hakuuleta msaada huu wa Malaika isipokuwa ni kwa ajili ya kuwapa bishara kwa msaada huo na ili nyoyo zenu zitulie na ziwe nzuri kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwenu. Na msaada wa hakika unatoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kushinda Ambaye Hashindwi, Mwenye hekima katika uendeshaji mambo Wake na matendo Yake.