Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:128

3:128
ليس لك من الامر شيء او يتوب عليهم او يعذبهم فانهم ظالمون ١٢٨
لَيْسَ لَكَ مِنَ ٱلْأَمْرِ شَىْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَـٰلِمُونَ ١٢٨
لَيۡسَ
لَكَ
مِنَ
ٱلۡأَمۡرِ
شَيۡءٌ
أَوۡ
يَتُوبَ
عَلَيۡهِمۡ
أَوۡ
يُعَذِّبَهُمۡ
فَإِنَّهُمۡ
ظَٰلِمُونَ
١٢٨
Wewe huna lako jambo katika haya - ama atawahurumia au atawaadhibu, kwani wao ni madhaalimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Huna, ewe Mtume, katika mambo ya waja chochote kile. Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Peke Yake, Asiyekuwa na mshirika. Na huenda, baadhi ya hawa waliokupiga vita, vifua vyao vikaufungukia Uislamu, wakasilimu na Mwenyezi Mungu Akazikubali toba zao. Na yule atakayesalia katika ukafiri wake, Mwenyezi Mungu Atamuadhibu duniani na Akhera kwa sababu ya udhalimu wake na uadui wake.