Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika Mbingu na vilivyomo katika Ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ni vya Mwenyezi Mungu Pekee vilioko mbinguni na vilioko ardhini; Anamsamehe Amtakaye kati ya waja Wake kwa rehema Zake na Anamuadhibu Amtakaye kwa uadilifu Wake. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasamehe madhambi ya waja Wake na ni Mwenye huruma kwao.