Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema; 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wale ambao wanatoa mali yao katika hali ya wepesi na uzito, na wanaozuia hasira zilizo ndani ya nafsi zao kwa kusubiri, na wanaowasamehe waliowadhulumu wanapokuwa na uwezo. Huu ndio wema ambao Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kuwa nao.