Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na bora ya malipo ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi Aliwapa Mwenyezi Mungu, wale wenye kusubiri, malipo yao duniani kwa kuwanusuru na maadui zao, kwa kuwafanya wakae kwa utulivu katika ardhi na kwa malipo mema yaliyo makubwa Akhera, nayo ni mabustani ya Peponi yaliyojaa neema. Na Mwenyezi Mungu Anampenda kila mtenda wema katika kumuabudu Mola wake na kuamiliana kwake na viumbe Wake.