Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:151

3:151
سنلقي في قلوب الذين كفروا الرعب بما اشركوا بالله ما لم ينزل به سلطانا وماواهم النار وبيس مثوى الظالمين ١٥١
سَنُلْقِى فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلرُّعْبَ بِمَآ أَشْرَكُوا۟ بِٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَـٰنًۭا ۖ وَمَأْوَىٰهُمُ ٱلنَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٥١
سَنُلۡقِي
فِي
قُلُوبِ
ٱلَّذِينَ
كَفَرُواْ
ٱلرُّعۡبَ
بِمَآ
أَشۡرَكُواْ
بِٱللَّهِ
مَا
لَمۡ
يُنَزِّلۡ
بِهِۦ
سُلۡطَٰنٗاۖ
وَمَأۡوَىٰهُمُ
ٱلنَّارُۖ
وَبِئۡسَ
مَثۡوَى
ٱلظَّٰلِمِينَ
١٥١
Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi yao ni Motoni; na maovu yaliyoje maskani ya wenye kudhulumu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Tutatia fazaa na hofu kubwa katika nyoyo za waliokufuru, kwa sababu ya kumshirikisha kwao Mwenyezi Mungu na wale wanaodaiwa kuwa ni waungu. Wao hawana dalili au hoja kuwa waungu hao wana haki ya kuabudiwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi hali yao hapa duniani ni papatiko na babaiko kwa kuwaogopa Waumini. Ama mahali pao watakaposhukia Akhera ni Moto. Na hili ni kwa sababu ya udhalimu wao na uadui wao. Na makao maovu kwao ni makao haya.